Kuhusu Mfumo wa Huduma za Ugani

Mfumo wa Ugani ni sehemu ya jukwaa la ubunifu wa kidijitali linalojulikana kama UGANI lililosheheni hazina ya maarifa yaliyotafitiwa ya kilimo na sayansi zinazohusiana na kilimo. UGANI ni mtandao wa kijamii unaotoa huduma za usambazaji wa taarifa kwa ushiriki ili kuboresha maisha ya jamii za vijijini nchini Tanzania na kwingineko.  Hili ni jukwaa la wafanyakazi wa Utafiti na Uendelezaji kilimo, watoa huduma, wakala wa ugani, wasaidizi wa maafisa ugani, wahudumu wa mifugo, wataalam wa mawasiliano na wawakilishi wa mashirika ya wakulima.

Mradi umeanzishwa, unaendelezwa na kusimamiwa na shirika lisilolenga kutafuta faida liitwalo ‘The GardenFarm Institute’. Taasisi hii inabuni, inapanga na kuongeza thamani ya taarifa nyingi zilizopo katika kilimo na sayansi ya viumbe hai ili kuzifanya zipatikane, zitumike na zilete manufaa na tija.

Wasiliana nasi

Anwani:

Mfumo wa Huduma za Ugani,
Morogoro,
S.L.P 6255,
Morogoro,Tanzania

Namba ya simu: +255 (739) 123 123 , +255 (624) 123123

Barua pepe: taarifa@ugani.or.tz